Na Joachim Mushi
TIMU ya Taifa ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) hatimaye imefanikiwa kuendelea ki-bahati nasibu na hatua ya pili katika Mashindano ya Kombe la Tusker Chalenji baada ya fufungwa mabao 2-1 na timu ya Taifa ya Zimbabwe jana katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kilimanjaro Stars imeponea chup chup baada ya kufanikiwa kufunga bao moja katika mchezo huo, iliyojikuta ikiupoteza na kubamizwa kwa mabao 2-1 na vijana wa Zimbabwe.
Goli la Kilimanjaro Stars lililofungwa kwa njia ya penati na mchezaji Mwinyi Kazimoto lilipatikana kipindi cha pili baada ya mchezaji wa Zimbabwe kumuangusha Mrisho Ngassa ndani ya 18 na muamuzi wa mchezo huo kuamuru ipigwe penati.
Kilimanjaro Stars imeingia hatua ya robo fainali ambapo, Desemba 6, 2011 itaingia dimbani kupepetana na Timu ya Taifa ya Malawi. Timu zilizoingia katika hatua hiyo kupitia kapu la ‘Best Looser’ ni pamoja na Zanzibar na Kilimanjaro Stars yenyewe.
magoli yote yalifungwa kutokana na safu ya ulinzi ya Stars kuzembea. Kwa ujumla katika kipindi hicho wachezaji wa Stars walionekana wakicheza kama wamelazimishwa vile.
Kili Stars-Juma Kaseja, Shomari Kapombe/Erasto Nyoni, Ibrahim Mwaipopo, Juma Jabu, Godfrey Taita, Juma Nyosso, Shaban
Nditi, Mrisho Ngassa, Said Maulid/Nurdin Bakari, Mwinyi Kazimoto/Hussein Javu, Thomas Ulimwengu na Ramadha Chombo.
Awali timu Kabla ya mchezo timu ya Taifa ya Kenya Harambee Stars ilifungasha virago katika mashindano haya baada ya kupata kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa maasimu wao wa kubwa timu ya Taifa ya Sudan. Kwa matokeo hayo timu ya Zanzibar imepata nafasi ya kuingia hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.