Prof. Mwandosya atoa shukrani kwa waliomuombea

Waziri wa Maji, Profesa Mark Mwandosya (kulia ) akizungumza na viongozi watendaji wakuu wa wizara hiyo pamoja na waandishi wa habari na kutoa shukrani kwa watu mbalimbali waliokuwa wakimjulia afya yake na kumwombea, akiwemo Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, viongozi wa dini na wengine wa kisiasa ambao ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, na Profesa Ibrahim Lipumba na wananchi Watanzania kwa ujumla bila kujali Itikadi za kisiasa. Kushoto ni Naibu Waziri wa wizara hiyo Gerson Lwenge.

Waziri wa Maji, Profesa Mark Mwandosya (wa pili kushoto) akiwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mhandisi Christopher Sayi (pili kulia) wakielekea katika ukumbi wa mikutano wizarani hapo kwa ajili ya kuzungumza na baadhi ya watendaji wakuu wa wizara na waandishi wa habari kutoa shukrani kwa watu mbalimbali waliokuwa wakimjulia afya yake na kumwombea. Wa kwanza kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Bashir Mrindoko, kushoto ni mtoto wa waziri, Emmanuel Mwadosya.

Viongozi Watendaji Wakuu wa Wizara ya Maji na waandishi wa habari wakimsiliza Waziri wa Maji, Profesa Mark Mwandosya wakati alipokuwa akitoa shukrani kwa watu mbalimbali waliokuwa wakimjulia afya yake na kumwombea. (Picha zote kwa hisani ya Wizara ya Maji)