Ngorongoro Heroes yaanza kwa sare

Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura

Na Mwandishi Wetu

TANZANIA (Ngorongoro Heroes) imeanza kwa sare michuano ya Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Kusini mwa Afrika (COSAFA) kwa vijana chini ya miaka 20 inayofanyika Gaborone, Botswana.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TFF, kupitia kwa Ofisa Habari wake, Boniface Wambura ni kwamba, mchezo wa Desemba 2 mwaka huu dhidi ya mabingwa watetezi Zambia uliofanyika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Gaborone, timu hizo zilitoka sare ya kufungana mabao 3-3.

Wambura alisema mabao ya Ngorongoro Heroes yalifungwa dakika ya 2 na 13 kupitia kwa Simon Msuva. Bao la tatu lilifungwa na Hassan Dilunga dakika ya 40. Evans Kangwa aliifungia Zambia mabao mawili wakati la kusawazisha lilifungwa na Alex Sichone.

Aidha ameongeza kuwa Ngorongoro iliwakilishwa na; Jackson Wandwi, Hassan kKessy, Issa Rashid, Samuel Mkomola, Frank Raymond, Atupele Jackson, Simon Msuva, Amani Kyata, Edward Shija, Frank Sekula na Hassan Dilunga.