Ethiopia, Djibouti na Somalia zaaga mashindano ya Tusker

Wachezaji wa timu ya Ethiopia wenye jezi za rangi ya njano na bukta za kijani wakijiandaa kuzuia moja ya mipira ya adhabu zilizokuwa zikielekezwa langoni mwao leo katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam timu hiyo ilipopambana na Malawi katika Mashindano ya Kombe la Tusker Chalenji. Timu hizo zilitoka suluu ya 1-1. (Picha na Joachim Mushi)

Na Mwandishi Wetu

TIMU za Somalia, Djibouti na Ethiopia leo zimeyaanga rasmi mashindano ya Kombe la Tusker Chalenji jijini Dar es Salaam yanayofanyika katika Uwanja wa Taifa nchini Tanzania

Somalia imekuwa ya kwanza kuaga mashindano hayo baada ya kufungwa michezo yote kwa jumla ya magoli 11. Timu za Djibouti yenyewe imeyaanga mashindano ya Tusker baada ya kukubali kichapo cha magoli 5-2, huku ikiwa aina hata pointi moja katika michezo yote na kufanya iondoke na kapu la magoli 10.

Timu ya Ethiopia imetolewa katika mashindano hayo baada ya kuambulia pointi mbili katika mchezo wake wa leo ilipotoka suluhu ya bao 1-1 na dhidi ya Malawi.

Kwa matokeo ya leo kati na Ethiopia, Malawi imepita kwa kuongoza kundi ‘C’ ikiwa imejinyakulia pointi saba huku Timu ya Taifa la Kenya ikishika nafasi ya pili kwa pointi tatu.

Timu ambazo tayari zimepita katika michuano hiyo ya makundi na pointi zao kwenye mabano ni pamoja na Rwanda (6), Uganda (6), Burundi (7), na Malawi (4).

Kesho michezo yote itakuwa na ushindani mkubwa kwani katika mchezo wa kwanza kati ya Kenya na Sudan yeyote aweza kuendelea iwapo atashinda katika mchezo huo. Kenya yenye pointi 3 ikishinda itafikisha pointi nne hivyo kufuzu mashindano hayo, wakati Sudan ina pointi moja moja ikishinda itafikisha pointi 4, hivyo kuweza endelea na mashindano hayo.