Dk. Bilal afungua mkutano wa viongozi TAKUKURU Tanga

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Takukuru, Edward Hosea, mara baada ya kufungua ramsi mkutano Mkuu wa mwaka wa siku mbili wa Viongozi wa Takukuru uliofunguliwa leo Novemba 28, mkoani Tanga.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati akifungua rasmi Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Viongozi wa Takukuru mkoani Tanga leo Novemba 28. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Takukuru, Edward Hosea (kushoto) ni Waziri wa Ofisi ya Rais-Utawala Bora, Mathias Chikawe.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Takukuru, Edward Hosea, wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Viongozi wa Takukuru, uliofanyika Mkoani Tanga leo Novemba 28. Kushoto ni Waziri wa Ofisi ya Rais - Utawala Bora, Mathias Chikawe. Picha na Muhidin Sufiani-OMR


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wakuu wa usalama wa Mkoa wa Tanga baada ya kufungua mkutano huo.