Na Mwandishi Wetu, Arusha
HATMA ya kesi inayowakabili viongozi wa juu wa CHADEMA, Katibu Mkuu, Wilbroad Slaa na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe itajulikana Desema 20, 2011- baada ya hakimu kumaliza usikilizaji wa pingamizi. Kesi hiyo pia inawajumuisha wabunge watatu pamoja na wafuasi wao 14, wa cha hicho.
Jana mjini hapa wakili wa Serikali alikuwa akijibu hoja za pingamizi zilizokuwa zimetolewa mwishoni mwa wiki iliyopita na wakili wa utetezi, juu ya Hati ya mashitaka. Mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha Hakimu, Charles Magesa, anayesikiliza shauri hilo alisema kuwa baada ya mahakama kusikiliza hoja za pande zote mbili mahakama hiyo inaahirisha shauri hilo hadi Disemba 20 ambapo itatoa uamuzi juu ya pingamizi hizo.
Shauri hilo namba 5 la mwaka huu, mahakama hiyo inatarajiwa kutoa
uamuzi kama watuhumiwa hao wana kesi ya kujibu au lah kwa kupitia
pingamizi zilizowasilisha na Wakili wa Utetezi Method Kimomogolo.
Kimomogoloa mwishoni mwa wiki iliyopita aliwasilisha pingamizi juu ya
hati ya mashitaka hayo ni ya kufikirika na hayajakidhi masharti ya
sheria.
Awali Wakili wa Serikali Edwin Kakolaki alidai mahakama hapo
kusikitishwa na hoja zilizotolewa na wakili wa Utetezi kwa madai kuwa
hoja hizo zilikuwa zimejaa siasa hazijakidhi matakwa ya kisheria.
“Mahakama hii ni ya kisheria zi ya kisiasa tulitegemea hoja ambazo
zingewasilishwa na wakili Msomi aliyebobea katika sheria kuwa angeweza kuwa na ueledi wa kutosha na kuleta hoja za kisheria na si hoja za kisiasa kama alizosilishwa mahakamani hapa,” alidai Kakolaki.
Aliieleza mahakama hiyo kuwa hati ya mashitaka inapaswa kukataliwa
iwapo ina mashaka ya aina yoyote na kudai kuwa katika hati hiyo ya
mashitaka hakuna sehemu yoyote inayoonyesha kuwa kuna mashaka.
Kakolaki alidai kuwa maelezo ya awali ya kosa siyo ushahidi, kwa mujibu wa sheria yanamsaidia mshtakiwa kufahamu mashitaka yanayomkabili huku ushahidi ukiwa bado haujawasilishwa mahakamani.
Alidai kuwa katika kosa la kwanza linalowakabili watuhumiwa wote la
Kula njama na kutenda makosa (6) ambapo wakili wa utetezi alidai kuwa
kwa mujibu wa sheria shitaka moja haliwezi kuwa na makosa sita ndani
yake na badala yake kila kosa linapaswa kujitegemea.
Alidai kuwa Kimomogolo alipotoka kwa kutokujua kiini cha kosa ambacho
ni kula njama ya kutenda makosa, katika hati hiyo watuhumiwa hao
wanadaiwa kula njama na kutenda makosa hayo, hati imeelezea ili
washitakiwa wajue makosa gani walikula njama kuyatenda.
Akizungumzia pingamizi nyingine zilizowasilishwa na Kimomogolo alisema kuwa Wakili huyo alikuwa anaoanisha maelezo ya hoja za awali na kuyachukulia kama ushahidi huku.
“Kinachoonekana kuletwa hapa na Kimomogolo ni ushahidi wakati bado
hatujafikia hatua ya ushahidi, Jamhuri inaona suala hili siyo la msingi tunachukulia kama siasa,”
“Tunasikitika Wakili badala ya kuleta hoja za kisheria anakuja na
mtazamo wake huku akidai mashitaka ni kuonea ambayo hayana mantiki
kisheria, ningemshauri asubiri tulete ushahidi na wao waje na utetezi
wao na mahakama kutoa maamuzi yake kwenye hukumu,” Alidai na kuongeza
Alidai kuwa pingamizi hizo za Utetezi halina nguvu ya kisheria hivyo
kuiomba mahakama hiyo itupilie mbali pingamizi hizo na Jamhuri
kuendelea na hatua ya ushahidi.
Kwa upande wake Kimomogolo akijibu hoja hizo, alipingana na Kakolaki na kudai kuwa maelezo aliyotoa siyo ya ushahidi na badala yake hati ya mashitaka inalenga kwenye ushahidi walionao upande wa wadai na siyo ushahidi unaokusanywa na upande wa wadai kwani hati inaandaliwa baada ya ushahidi kukamilika.
Alidai kuwa maelezo ya awali ni muhtasari wa ushahidi wa kesi kwa
mujibu wa kifungu cha sheria cha 193 (4) cha sheria ya mwenendo wa
mashitaka ya jinai.
Kimomogolo aliiomba mahakamani hiyo kukataa ombi la Kakolaki kwa
madai kwua mahakama itakuwa “imekanyaga” haki kwa washitakiwa hao kwani hati haionyeshi kosa lolote chini ya sheria na upande wa Serikali kufanya upelelezi upya na kufungua kesi nyingine.