Wahariri wawasili Moshi kushiriki uzinduzi wa kiwanda cha SBL

Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakiwasili mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro wakitokea jijini Dar es Salaam tayari kwa kushiriki uzinduzi a kiwanda kimpya cha kampuni ya Bia ya Serengeti Breweries (SBL).

Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro

JUKWAA la Wahariri Tanzania (TEF) limewasili mjini Moshi leo mchana kwa ajili ya kushiriki kwenye hafla ya uzinduzi wa Kiwanda kipya cha Kampuni ya Bia ya Serengeti Breweries (SBL) kinachozinduliwa kesho mkoani Kilimanjaro.

Akizungumza na dev.kisakuzi.com Katibu Mkuu wa TEF, Boniface Meena amesema jumla ya wahariri 36 kutoka vyombo vya habari mbalimbali nchini wamewasili tayari kwa kushiriki katika uwekezaji huo mkuwa wa kiwanda mjini hapa.

Mhariri wa gazeti la The Guardian, Wence Mushi (kushoto) akibadilishana mawazo na mhariri wenzake wa gazeti la The Guardian on Sunday, Richard Mgamba (kulia)- wahariri hawa nguli ni miongoni mwa wahariri waliowasili Moshi kushiriki katika hafla ya uzinduzi wa kiwanda cha SBL mkoani Kilimanjaro. (Picha zote na Joachim Mushi)


Akizungumzia tukio hilo, Meena amesema wanashukuru kampuni ya SBL kuamua kuwaalika wao kuwa sehemu ya wageni waalikwa ambao watahudhuria hafla hiyo ambayo ni muhimu kwa maendeleo ya Mkoa wa Kilimanjaro kimapato.

“Kwa kweli tumeshukuru kupewa nafasi hiyo na SBL ya kushuhudia uzinduzi wa kiwanda hicho. Tunaamini SBL wanatambua mchango wengu ndio maana wametualika…na hii ni kama wametimiza ahadi yao kwani tuliwahi kukitembelea kiwanda hiki kikiwa kinajengwa na leo tunashuhudia uzinduzi,” alisema Meena.

Uzinduzi wa kiwanda hicho unatarajiwa kufantika kesho kuanzia majira ya saa tatu, hafla ambao inatarajiwa kuhudhuriwa na wangeni mbalimbali wakiwemo viongozi.