Ujumbe Mkali wa Rais Magufuli kwa Wakuu wa Mikoa Wapya Leo…!

Ujumbe Mkali wa Rais Magufuli kwa Wakuu wa Mikoa Wapya Leo...!

HAYA ndio maneno ambayo Rais John Pombe Magufuli amewaambia wakuu wa mikoa wapya baada ya kuwaapisha leo Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais John Magufuli ameaambia wahakikishe vijana wanafanya kazi na kuacha uzembe.

Rais Magufuli amewataka wa kuu wa mikoa kuhakikisha hakuna vijana ambao watakuwa wanakwenda kucheza pool table asubuhi na badala yake vijana hao wanatakiwa kufanya kazi kweli kweli hata kwa kulazimishwa.

“Nimeamua kuwateua wakuu wa mikoa nikiamini kwamba mtaniwakilisha vizuri katika mikoa yenu, Napenda niwape pole kwa sababu mtakwenda kufanya kazi kweli kweli kutatua kero za wananchi wetu. Lakini pia niwaombe wakuu wa mikoa mkasimamie watu wafanye kazi hasa vijana haiwezekani vijana leo hii unamkuta saa mbili asubuhi anacheza Pool table wakati wa kina mama wanalima shambani, kama hawataki kufanya kazi kwa kupenda walazimishwe kufanya kazi.

“…Nimeamua kuwateua nyinyi kama wakuu wa mikoa nikiamini mtaniwakilisha vizuri popote. Rais Magufuli: Wananchi Kusindikizwa na polisi maana yake hakuna usalama. Na hasa kutambua nyinyi ndio wenyekiti wa kamati za ulinzi na usalama mkaniwakilishe.

Rais Magufuli; anasema haiwezekani kwa nchi ambayo inajitawala miaka 50 raia wake wakisafiri wasindikizwe na polisi wenye mitutu ya bunduki. Nataka Tanzania katika awamu yangu isitokee mahali mkuu wa mkoa anaomba chakula. Niwape grace time ndani ya siku 15 wakurugenzi wawe wamejumlisha wamewatoa wafanyakazi hewa katika payroll,” alisema

Rais Magufuli; anasema mshahara wa mwezi tukigundua mkurugenzi amelipa mshahara hewa ajue hana kazi na tunampeleka mahakamani Rais Magufuli: Singida na Dodoma ina wafanyakazi hewa 202…Leo pia tumeapisha Kamishna mkuu wa TRA na kamanda wa TAKUKURU.

Nyinyi mna mamlaka ya kuwaweka watu ndani hata masaa 48 wekeni watu ndani ili wajue mnatakiwa kuheshimiwa. Tusiogope kuchukua maamuzi, nafuu uchukue maamuzi hata kama ni mabaya yatarekebika huko mbele.

Rais Magufuli: Haiwezekani kila siku majambazi, kwa nini Rwanda hakuna majambazi, kwa nini Tanzania tu, mkafanye kazi. Magufuli: Morogoro watu wanauana sana ndio maana sikuona sababu ya mkuu wa mkoa kubaki pale.