Wahariri TEF Watembelea Mgodi wa Tanzanite One Mererani

Modest Apolinary Meneja na Kaimu Mkurugenzi wa mgodi wa Tanzanite One akiongozana na wahariri wa vyombo vya habari mara baada ya kujionea mipaka ya mgodi

Modest Apolinary Meneja na Kaimu Mkurugenzi wa mgodi wa Tanzanite One akiongozana na wahariri wa vyombo vya habari mara baada ya kujionea mipaka ya mgodi

 

01

Modest Apolinary Meneja na Kaimu Mkurugenzi wa mgodi wa Tanzanite One akiwaomyesha wahariri mbalimbali wa vyombo vya habari mipaka ya mgodi huo, wakati wahariri hao walipoutembelea mgodi wa huo uliopo Mererani wilayani Simanjiro katika mkoa wa manyara kwa ajili ya kuangalia na kujifunza kuhusu shughuli mbalimbali zinazoendeshwa katika mgodi huo ambao kwa sasa unamilikiwa na kampuni ya watanzania inayoitwa Sky Asocciate.

Mgodi huo unaendeshwa kwa ubia pamoja na shirika la madini la STAMICO, Bw. Modest Apolinary amelalamikia kampuni ya Bw. Said Nasoro maarufu kama (Mwarabu) kwa kuingia kwenye eneo la Tanzanite One la Kitalu C chini kwa chini na kukutana na njia za mgodi wa kampuni ya Tanzanite One maarufu kama (mtobozano) jambo ambalo limeifanya kampuni ya Tanzanite One kufunga baadhi ya migodi yake kwa sababu za kiusalama na uchimbaji usio na tija. 

2

Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakielekea Mererani kwa ajili ya kutembelea mgodi wa Tanzanite One mkoani Manyara leo.

4

Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakitembelea na kujionea baadhi ya migodi ya Tanzanite One katika Kitalu C iliyofungwa kutokana na kuingiliwa na wachimbaji wadogo.

5

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri TEF, Theophil Mkubga akiongoza wahariri wenzake ili kujionea mipaka ya kampuni ya Tanzanite One iliyoingiliwa na wachimbaji wadogo.

6

Mkuu wa Usalama wa kampuni ya Tanzanite One Bw. George Kisambe akiwaonyesha wahariri mipaka ya mgodi huo.

7

Mkuu wa Usalama wa kampuni ya Tanzanite One Bw. George Kisambe akiwaeleza jambo wakati akiwaonyesha wahariri mipaka ya mgodi huo.

11

Modest Apolinary Meneja na Kaimu Mkurugenzi wa mgodo wa Tanzanite One akiwaomyesha wahariri wa vyombo vya habari mipaka ya mgodi huku kwa mbali ukionekana mgodi uliofungwa mbele yao mgodi huu upo kitalu C na unapakana na Kitalu D cha wachimbaji wadogo.

14

Mhandisi Kimonge Kiravo akizungumza na Mhariri wa gazeti la Mwananchi Bw. Rashid Kejo.

15

Huu ni mmoja wa mitambo ya kuchakata mchanga wa madini mbalimbali ikiwemo Tanzanite katika mgodi huo.

16

Irene Mark Mhariri wa Gazeti la Tanzania Daima akishiriki kazi ya kuchambua madini ya Tanzanite wakati wahariri walipotembelea kiwandani hapo.

ONE5

Mmoja wa wafanyakazi wa kiwanda hicho akiendelea na kazi.

17

Baadhi ya wafanyakazi wakiendelea na kazi katika mtambo wa kuchambua madini ya Tanzaniate.

ONE3

Mkurugenzi mtendaji wa Fullshangweblog Bw. John Bukuku pamoja na Mhandisi wa mgodi wa Tanzanite One Bw. Anton Potigieter ambaye ni Meneja wa uchimbaji wa madini chini ya Ardhini wakiwa wamevalia mavazi rasmi tayari kwa kushuka mgodini mita 610 kwa ajili ya kujionea shughuli za uchimbaji zinavyofanyika.

ONE4

Mkurugenzi mtendaji wa Fullshangweblog Bw. John Bukuku akiwa katika picha ya pamoja na wahariri kutoka kulia ni Neville Meena Katibu wa TEF na Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima, Jimmy Charles kutoka Gazeti la Rai na kushoto ni Rashid Kejo Mhariri kutoka Gazeti la Mwananchi wakiwa wamevalia mavazi rasmi tayari kwa kushuka mgodini Mita 610 ili kuona shughuli za uchimbaji madini ya Tanzanite.

ONE2

Tukiwa tayari kuingia mgodini katikati ni Mzee Theophil Makunga Mwenyekiti wa Jukwaa wa la Wahariri TEF.

ONE1Mmoja wa wachimbaji akiendelea na kazi chini ya Ardhi mita 610 katika mgodi wa Tazaniate One uliopo Kitalu C.

ONE10

Mhariri wa Clouds FM, Joyce Shebe akishuka kwenye kiberenge mara baada ya kuwasili na wenzake mgodini mita 610 chini ya ardhi.

ONE12

Baadhi ya wanahabari wakipata maelezo katika mgodi huo kutoka kwa mmoja wa wasimamizi wa uchimbaji madini.

ONE13

Wachimbaji wakiendelea na kazi mgodini.

ONE6

Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali pamoja na baadhi ya wahandisi wa kampuni ya Tanzanite One walioongozana nao wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kurejea juu kutoka mgodini walipoutembelea mgodi huo.