Simba Sc Yaanza Kuota Ubingwa, Azam Yapanda Kileleni

simba

Klabu ya Simba imefanikiwa kuwa na matokeo mazuri tangu kikosi hicho kiwe chini ya Kocha raia wa Uganda Jackson Mayanja, Baada ya jana kuilaza JKT Ruvu Mabao 2-0. Magoli ya Hamisi Kiiza na Daniel Lyanga ya kuipa Simba pointi tatu kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya JKT Ruvu uliochezwa kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

Kiiza alipachika bao la kwanza kwa mkwaju wa penati baada ya Daniel Lyanga kuangushwa kwenye eneo la 18 la JKT Ruvu kisha mganda huyo kuukwamisha mpira kambani ikiwa ni dakika ya nane kipindi cha pili.

Dakika ya 27 kipindi cha pili, Daniel Lyanga aliihakikishia Simba ushindi baada ya kupachika bao la pili na la ushindi akitumia makosa ya mabeki wa JKT Ruvu waliokuwa wakiugombe mpira mrefu uliopigwa kutoka eneo la Simba. Mabeki hao walishindwa kuudhibiti mpira huo hatimaye ukamkuta Lyanga ambye moja kwa moja aliuweka wavuni.

simb

Ushindi wa huo unaifanya Simba kufikisha pointi 33 nyuma ya mahasimu wao Yanga bado wanapointi zao 36 huku wakisubiri kucheza mechi yao ya kesho dhidi ya Majimaji wakati Azam yenye pointi 39 inakaa kileleni mwa ligi baada ya ushindi wa jana dhidi ya Mgambo JKT uliochezwa jijini Tanga.

Jumla ya michezo mitatu ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara ilichezwa kwenye viwanja vya miji tofauti.
Mgambo JKT 1-2 Azam FC (Mkwakwani Stadium-Tanga)
Ndanda FC 4-1 Mbeya City (Nangwanda Sijaona-Mtwara)
Standa United 2-1 Toto Africans (Kambarage Stadium-Shinyanga)
Tanzania Prisons 2-1 Coastal Union (Sokoine Stadium-Mbeya)

leo itapigwa michezo mingine mitatu kwa ajili ya kukamilisha duru la kwanza la ligi kuu Tanzania bara ambapo mechi hizo zitakamilisha mechi 15 za kwanza za ligi msimu huu kisha kupisha ratiba ya michuano ya FA kisha kuanza kupigwa michezo mingine ya lala salama ya ligi hiyo.

Ratiba ya mechi zitakazopigwa leo ni kama ifuatavyo:
Mwadui FC vs Kagera Sugar
African Sports vs Mtibwa Sugar
Yanga SC vs Majimaji FC