Mnyama Ngiri akiwa amejipumzisha kwenye tope kama alivyokutwa na kamera yetu |
Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) wamefanya ziara ya siku mbili ya kitalii katika hifadhi ya taifa ya Saadani pamoja na sehemu ya kihistoria ya Kaole iliyopo Bagamoyo ikiwa ni sehemu ya kujifunza pamoja na kuhamasisha utalii wa ndani.
Wanafunzi hao kutoka katika “Collage” tofauti tofauti ikiwemo utalii , uchumi na biashara waliofanya ziara hiyo ikiwa chini ya mwamvuli wa University of Dar es Salaam Tourism Association (DUTA), walipata fursa ya kujifunza na kushuhudia wanyama pori pamoja na sehemu ya kihistoria ya Kaole na kuhamasisha jamii hasa ya wasomi kuwa mfano wa kuigwa kwa kuzuru hifadhi pamoja na makumbusho ili kuhimiza utalii wa ndani.
Hii ni tabia ya kipekee ya ngiri ambapo hula nyasi akiwa amepiga mfano wa magoti kwa kukunja miguu ya mbele |
Mtembezi na muelekezi katika hifadhi ya Saadani Bw.Mollel akifafanua jambo wakati wa ziara ndani ya hifadhi |
Baadhi ya wanafunzi wakisikiliza historia kuhusu mji huu wa Saadani huku toka kwa mwenyeji na mkongwe wa eneo hilo mzee Mlelwa (mwenye shati la kijani) wakati wa jioni |
Mambo ya Msosi: baadhi ya wanafunzi wakiwa katika harakati za kuchoma kitoweo kwa ajili ya mlo wa usiku
|
wanafunzi hao wakiwa karibu na eneo ambalo maji kutoka mto wami yanakutana na maji ya bahari ya hindi |
Kwa umakini na huku wakipewa fursa ya kuuliza maswali , wakisikilza historia ya eneo la Kaole na mfululizo wa matukio ya kihistoria kutoka kwa mtaalamu wa historia Bw.Ramadhani |
Moja kati ya mamba wanaopatikana katika eneo la Kaole Mamba Ranch |
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakiwa mbele ya msikiti wa kwanza uliojengwa katika pwani ya Afrika ya mashariki |
Kulingana na historia ya eneo hili ,inasemekana kuwa mbuyu huu umeishi zaidi ya miaka mia tano na wengi wamekuwa wakiamini kuuzunguka mbuyu huu (kutoka upande wa kushoto kwenda kulia) kunaweza kumuongezea mtu miaka ya kuishi. Picha na Dickson Mulashani wa FUNGUKA LIVE MEDIA |