Aliyekuwa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo na Makazi, Angela Kairuki (kushoto), akizinduwa DVD ya nyimbo za injili iitwayo Sogea wakati wa uzinduzi wa albamu mbili za
nyimbo hizo ikiwepo na ya Baraka za Bwana zilizoimbwa na muimbaji Anna Shayo Dar es Salaam juzi. Kulia ni Mwanaharakati Hoyce Temu na mwimbaji na mmiliki wa albam hizo, Anna Shayo. Kairuki alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo.
Mwimbaji na mmiliki wa albam hizo, Anna Shayo (kulia), akimkabidhi Kairuki risala yake.
Waziri Kairuki akimkabidhi Anna Shayo kitita cha sh.milioni moja.
Mwimbaji wa nyimbo za injili, Juvenalister Mabumba akitoa burudani katika uzinduzi huo.
Mwimbaji wa nyimbo za injili, Ulimbaga Mwakatobe akiimba wakati wa uzinduzi huo.
Mwimbaji Andrew Kihwelu (kushoto), akitoa burudani.
Mwimbaji Supa Belgano (kulia), akitoa burudani.
Kairuki akisalimiana na waimbaji wa nyimbo za injili.
Mwimbaji, Stellah Joel (kulia), akiimba katika uzinduzi huo huku akisindikizwa na wenzake.
Meza kuu ikipiga makofi. Kushoto ni Baba Askofu, Redoice Ndalima.
Muimbaji Anna Shayo akiimba wakati akizitambulisha nyimbo zake zilizomo katika albam hiyo.
Anna Shayo na wacheza shoo wake wakipagawisha.
Picha zikipigwa katika uzinduzi huo.
Mwimbaji Anna Shayo akiwa na waimbaji wenzake.
Hapa ni shangwe na furaha wakati wa uzinduzi.
Baadhi ya waimbaji wa nyimbo za injili.
Ni kuserebuka kwa kwenda mbele ndani ya yesu.
Wageni waalikwa na waimbaji wa nyimbo za injili wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Na Dotto Mwaibale
SERIKALI imesema itaendelea kuwaunga mkono wasanii mbalimbali ambao tungo zao zitakuwa zinadumisha upendo na amani ya nchi.
Hayo yalibainishwa na aliyekuwa Naibu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela Kairuki wakati akizindua albam mbili za nyimbo za injili za Sogea na Baraka za Bwana za muimbaji Anna Shayo.
“Serikali itaendelea kuwajengea miundombinu mizuri wasanii ambao tungo zao zinahamasisha jamii kudumisha amani na upendo hivyo kuifanya nchi kutulia kupitia nyimbo zao” alisema Kairuki.
Kairuki alisema mbali ya nyimbo hizo kuhamasisha jamii kuitunza amani ya nchi pia zimekuwa zikiburudisha na kuhubiri habari njema hivyo kuwaidia wananchi kuwajenga kimaadili.
Kwa upande wake mmiliki wa albam hizo mwimbaji wa nyimbo za injili Anna alisema sehemu ya mapato atakayopata baada ya kuuza DVD hizo ambazo zipo katika maduka ya Msama Promotion atazitumia kuwasaidia watoto yatima wenye ulemavu wa akili wanaolelewa katika Kituo cha Lushoto mkoani Tanga katika kipindi hiki cha Sikukuu ya Krismas.
Alisema pamoja na kusaidia kituo hicho pia anahitaji kupata sh. milioni 25 ili kununua vyombo vya kupazia sauti ili aweze kupanua huduma yake ya uimbaji na kuhubiri.
Katika uzinduzi huo Kairuki alitoa sh.milioni 1 kwa ajili ya kumuunga mkono mwimbaji huyo ili kupata fedha za kununulia vyombo hivyo ambapo pia wageni waalikwa waliweza kumchangia.