Wadau na Mashabiki wasoka jijini Arusha waeelezwa kusikitishwa na mwenendo wa timu yao ya AFC kutokana na kupoteza michezo yake yote mitatu tangu msimu wa ligi daraja la pili uanze.
Mwishoni mwa timu ya AFC ililala kwa bao 1-0 dhidi ya JKT Rwankoma mchezo uliopigwa katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, huku mashabiki walioshuhudia mpambano huo wakiwa na huzuni kubwa kutokana na kiwango kibovu kilichoonyeshwa.
Wakizungumza mara baada ya mpambano huo kumalizika ,Mmoja wa mashabiki hao Edwini Myuka alieleza kuwa mwenendo mbovu wa timu ya AFC kwanza unasababishwa na wachezaji wenyewe kutoonyesha ushirikiano kwani wamekuwa wakipata nasafi na kushindwa kuzitumia ipasavyo.
“Kweli soka la Arusha limeendelea kuwa chini pia likisababishwa na uongozi wa chama cha mpira mkoani hapa kushindwa kutoa ushirikiano kwa timu hii ya wakazi wa jiji la Arusha pasipo kuwaonyesha ushirikiano wa aina yeyeote kwani timu imekuwa ikijiendea yenyewe tu ikionekana kukata tamaa.”alieleza Myuka.
Shabiki mwingine Ally Mohamed Ally alisema kiwango cha timu cha AFC kimeshuka sana ukilinganisha hapo awali Kutokana na wadau mbalimbali wa soka kushindwa kabisa kuiunga mkono,Kinachotakiwa timu ikae chini iweze kujipanga upya msimu ujao.
Omary Habiby aliweza kuiandikia timu yake ya JKT Rwamkomna bao moja na la pekee lililodumu kwa dakika 90 za mchezo baada ya kuachia shuti kali lililokwenda moja kwa moja nyavuni.
Kocha wa timu ya JKT Rwamkoma Said Ally Mbwana alisema kuwa Nidhamu ya mchezo imeisaidia timu yake kuweza kuibuka na ushindi wa kwanza tena ugenini kutokana na wachezaji kuonyesha kujituma zaidi tangu mpira ulipoanza.
Hata hivyo timu ya AFC Imepoteza michezo yake mitatu iliyocheza tangu kuanza kwa ligi ikiwemo michezo yake iliyocheza na timu ya Pamba ya jijini Mwanza na kufungwa mabo 2-0 ,vile vile ilifungwa na timu ya Alliance Spors Academy pia ya Mwanza mbao 3-0 .