Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli akiwaambia wananchi wa Karatu katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Bwawani, kuwa mmoja wa viongozi wa upinzani anayempenda kwa dhati, ni aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dkt Wilbrod Slaa,amesema kuwa ni kiongozi imara asiyependa kuyumbishwa na kwamba ni kiongozi mwenye msimamo thabiti na mapenzi makubwa na nchi yake Tanzania.
Umati wa Washabiki na wafuasi wa CCM waliokusanyika katika uwanja wa Bwawani jioni ya kwenye mkutano wa kampeni jioni ya mjini Karatu,wakishangilia mara baada kumsikiliza sera zake wakati akijinadi na kuomba ridhaa ya kuiongoza nchi katika kipindi cha awamu ya tano kwa nafasi ya Urais.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwanadi wagombea Viti vya Udiwani mbele ya umati wa wakazi wa mji wa Karatu jioni ya kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Bwawani mjini humo mkoani Arusha.
Wabunge wa viti maalum wanaowakilisha wanawake watarajiwa kutoka CCM kutoka mkoa wa Arusha, kushoto ni Catherine Magige na Violet Mfuko.
Mgombea Uubunge jimbo la Karatu Dk.Wilbald Slaa Lorri akimuombea kura Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli pamoja na yeye mbele ya wakazi wa mji wa Karatu jioni ya kwenye mkutano wa kampeni,kulia kwake ni Wabunge watarajiwa viti maalum wanaowakilisha wanawake mkoa wa Arusha, kushoto ni Catherine Magige na Violet Mfuko wakishangilia.
Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli pichani kushoto akiungana na wasanii Chege na Temba kucheza muziki wakati wa mkutano wa kampeni mjini Karatu, mkoani Arusha.
Mgombea urais wa Tganzania kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi katika mkutano wa kampeni mjini Mbulu, mkoani Manyara.
Dkt. Magufuli akisisitiza jambo mbele ya maelfu ya wananchi wa Mbulu jijini jioni ya kwenye mkutano wa kampeni.
Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akiwanadi wagombea ubunge na madiwani mbele ya wakazi wa mji wa Mbulu kwenye mkutano wa kampeni.
Dk Magufuli akijinadi kwa wananchi katika Mji wa Haydom, wilayani Mbulu, Manyara ambapo aliwataka wananchi kutowachagua wagombea wanaotoa rushwa kwani wakikubali wanaweza wakawauza wao na Tanzania kwa ujumla
Wakazi wa Haydom wakifuatila hotuba ya Dk Magufuli alipokuwa akiwahutubia kwenye mkutano wa kampeni mapema mchana mjini humo.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk . John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge Jimbo la Mbulu Vijijini, Fratei Masay mjini Haydom.
Washabiki na wafuasi wa CCM wakiwa na bango lao la ujumbe maridhawa kabisa.
Washabiki na wafuasi wa CCM wakishangilia ujio wa Dk Magufuli na kuwahutubia kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Bwawani mjini Karatu,mkoa wa Arusha. PICHA NA MICHUZI JR-KARATU