ABIRIA zaidi ya 54 wamenusurika kifo baada ya basi la Ngorika
walilokuwa wakisafiria kutoka Arusha kwenda jijini Dar es Salaam kupinduka
eneo la Kwa Mrefu majira ya saa 12:10 jana asubuhi,nje kidogo ya mji wa Arusha
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa
Arusha, Liberatus Sabas, alisema katika ajali hiyo, abiria mmoja
Hashim Mohammed (31), mkazi wa Mwanza
alijeruhiwa na amelazwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru.
Kamanda Sabas alisema kuwa uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa chanzo
cha ajali hiyo kilikuwa ni utelezi uliotokana na mvua iliyonyesha na
dereva kushindwa kushika breki,na alipofanikiwa kushika breki gari
lilianguka huku magurudumu yakiwa juu.
Alisema basi hilo lenye namba za usajili T 580 BBL, aina ya
Utong,lilikuwa likienedshwa na dereva aliyefahamika kwa jina la Nuru
Mdee (45) mkazi wa Dar es Salaam, anashikiliwa na polisi.
Alifafanua kuwa baada ya mahojiano na upelelezi kukamilika,devera huyo
anaweza kufikishwa katika vyombo vya sheria na kuwahimiza madereva
kuwa waangalifu wanapokuwa barabarani.