Mafunzo ya Habari za Migogoro kwa Wanahabari Yaanza Burundi

Waandishi wa habari kazini

Waandishi wa habari kazini


 
Na Isaac Mwangi, EANA – Arusha

WAANDISHI wa habari 30 kutoka nchi wananchama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wameaanza mafunzo juu ya uandishi wa habari za migogoro nchini Burundi Ijumaa. Mkuu wa Idara ya Mawasiliano ya Umma wa EAC, Richard Owora aliwaambia waandishi wa habari kuwa mafunzo hayo ya awamu hii, yamefanya waandishi wa habari waliokwishapata mafunzo juu ya mtangamano wa EAC kufikia 100.

“EAC inapania kutoa mafunzo zaidi kwa waandishi wa habari wa Afrika Mashariki kuhakikisha kwamba habari kuhusu jumuiya hiyo zinaadkiwa kwa uwiano, uhakika na kwa weledi unaostahiki,” alisema.

Katika hotuba yake iliyosomwa na Mtaalamu wa Habari wa EAC na Shirika la Kimataifa la Misaada la Ujerumani GIZ, Sukhdev Chhatbar, Owora alitoa wito kwa waandishi wa habari kuongeza kiwango cha habari za EAC katika vyombo vyao ili kuwa na jumuiya yenye uelewa mpana wa mambo yake ya mtangamano.

Mafunzio hayo yanayotarajiwa kumalizika Novemba 12, yatafuatiwa na mkutano wa EAC kuhusu Amani na Usalama, utakaofanyika kwa mudawa siku tatu kuanzia Novemba 13-15. Waandishi hao watashiriki pia mkutano huo ambao pamoja na mambo mengine utawaleta pamoja wataalamu 150 wa sekta ya amani na usalama, wapigania haki za kiraia,viongozi wa dini na mawaziri.

Wengine watakaohudhuria mkutano huo ni pamoja na mashirika yaisiyo ya kiserikali, vijana, wanasiasa, wanawake, na maofisi wengine kutoka wizara za husika na masuala ya jumuiya.