Dk Shein: Wanao Potosha Falsafa ya Mwenge Hawatutakii Mema

Dk. Shein alisisitiza kuwa Tanzania imeweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kuleta ukombozi wa kweli katika nchi zote za Kusini mwa Afrika ambazo zilikuwa zikitawaliwa na wananchi wake kubaguliwa kwa misingi ya rangi zao.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein amezindua mbio za Mwenge wa Uhuru na kuwaeleza wananchi wa Tanzania kuwa Mwenge wa Uhuru hauna uhusiano na dini, wala chama cha siasa.
 
Dk. Shein aliyasema hayo leo huko Chokocho, Mkoa wa Kusini Pemba katika uzinduzi wa mbio za mwenge wa Uhuru.
 
Katika hotuba yake, Dk. Shein alieleza kuwa huo ni mwenge wa Serikali na upo kwa kutimiza malengo yake na ndio maana zimekabidhiwa Wizara mbili kuziratibu shughuli zake moja kutoka SMZ na nyengine kutoka SMT.
 
Alisema kuwa Katiba zote mbili zimeeleza kuwa Serikali zote hazina dini, isipokuwa wananchi wake ndio wana dini zao mbali mbali na Serikali inaziheshimu sana na itaendelea kuziheshimu na wala hazitaingilia uhuru wa kuabudu wa mtu yeyete, isipokuwa jambo la msingi na la kuzingatia ni kuwa taratibu na sheria za nchi zifuatwe.
 
“Watu wanapotosha falsafa ya mwenge tuwatamnbue vizuri kuwa hawatutakii mema.. Dhamira yao ni kuturejesha nyuma tunakotoka”, alieleza Dk. Shein.
 
“Hawapendi hata kidogo kuona Tanzania inasonga mbele kwa mafanikio kutokana na umoja wake na wananchi wake kuishi kwa amani, upendo na utulivu na wanapata maendeleo yao, napenda kutoa wito tuendelee kuishi kwa umoja na kupendana”.alisisitiza Dk. Shein.
 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Mohamed Shein,akivalishwa skafu na Kijana Asia Ibrahim,alipowasili
katika sherehe za uzinduzi wa mbio za  Mwenge wa Uhuru  Kitaifa huko
Chokocho Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba leo,(katikati) Waziri
wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Tanzania Bara,Dk.Fenelle
Mukangara, .[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]


Aidha, Dk. Shein aliwasihi vijana wote nchini kushirikiana vyema na viongozi wao na Serikali zote mbili zilizopo madarani na kuwaeleza kuwa mustakabali wa Tanzania ni mzuri na ni wa kupigiwa mfano duniani kote.
 
Dk. Shein alisema kuwa Mwenge wa Uhuru, tangu kuasisiwa kwke miaka 50 iliyopita, umelet mafanikio makubwa hapa nchini pamoja na nchi zilizo jirani na nchi za Kusini mwa Afrika wakati wa ukombozi wan chi hizo.
 
Alisema kuwa kupitia Mwenge wa Uhuru kazi kubwa imefanyika katika kuhubiri amani na utulivu na kuzitangaza Sera hizo kwa Watanzania wote.
 
Dk. Shein alisisitiza kuwa Tanzania imeweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kuleta ukombozi wa kweli katika nchi zote za Kusini mwa Afrika ambazo zilikuwa zikitawaliwa na wananchi wake kubaguliwa kwa misingi ya rangi zao.
 
“Watanzania tumepata heshima kubw na tuna haki ya kujivunia juu ya hatua hiyo kwani tumejenga historia mpya ya Bara la Afrika ambayo haiwezi kusahaulika duniani kote”,alisema Dk. Shein.
 
Aidha, alieleza kuwa mbali ya mafanikio hayo, Mwenge wa Uhuru umefanya kazi kubwa ya kupeleka ujumbe kwa Watanzania ili kupambana na rushwa, dawa za kulevya, ukimwi na unyanyasaji wa watoto na wanawake, ili kujenga Taifa lenye kuthamini haki, afya bora na heshima kwa kila mwanaadamu.
 
Kwa maelezo ya Dk. Shein Mwenge wa Uhuru umehamasisha wananchi kupambana na ujinga wa kutojua kusoma na kuandika na kuhimiza kufunguliwa kwa madarasa ya elimu ya watu wazima ili kutoa fursa ya kila mtu kujielimisha na kujiendeleza ili kuondokana na ujinga.
 
Mbio za mwenge wa uhuru wa mwaka huu una ujumbe wa mbambo muhimu kwa Watanzania yakiwemo Mapinduzi ya Zanzibar kutimiza miaka 50 ifikapo tarehe 12 Januari 2014, chini ya kaulimbiu ‘Tudumishe amani , tudumishe umoja, tulete maendeleo, Mapinduzi Daima’, Ushiriki na Ushirikishwajiw a vijana katika shughuli za maendeleo, Mapamban dhidi ya rushwa, ukimwi na dawa za kulevya.
 
Mbio hizo za zinatarajiwa  kufanyika katika Mikoa yote 30 na Halmashauri 161 ambapo Mwenge huo unatarajiwa kumaliza mbio zake Oktoba 14 mwa huu huko Iringa Tanzania Bara.
 
Mapema Mawaziri kutoa Wizara husika za SMT na SMZ walieleza pongezi zao kwa mafanio makubwa yaliopatikana na mashirikiano ya maandalizi ya uwashaji wa mwenge huo na kutoa pongezi za pekee kwa Dk. Shein kwa kendelea kuongoza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar iliyo chini ya Umoja wa Kitaifa kwa ujasiri mkubwa.
 
Viongozi mbali mbali walihudhuria katika sherehe hizo za uzinduzi wa mwenge wa uhuru akiwemo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd pamoja na viongozi wengine wa SMT na SMZ.
 
Nyimbo, ngoma na tumbuizo mbali mbali zilitumbuiza katika sherehe hizo.
 
Wakimbiza Mwenge huo wa Uhuru kwa mwaka huu jumla yao ni vija sita wakiongozwa na Juma Ali Simai kutoka Kusini Unguja na wengine ni Zamda John kutoka Tanga, Christopher Emmanuel kutoka Kigoma, Seperatus Lubinga kutoka Iringa, Zuwena Abdalla kutoka Kusini Unguja na Mgeni S. Mgeni