Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Profesa Rwekaza Mukanda (kulia) akibadilishana mawazo na Waziri Mkuu Mstaafu wa Uganda Profesa Apolo Nsibambi (katikati) na Balozi wa Zambia nchini Judith Kangoma( kushoto) jana mjini Dar es salaam wakati wa kongamano la siku moja la wanataalum liloandaliwa maalum na Chuo Kikuu cha Dar es salaam la kutambua mchango wa Profesa Goran Hyden alioutoa ndani na nje Tanzania
Goran -- Mwanataalum mkonge Profesa Goran Hyden (kushoto) akibadilishana mawazo na Balozi wa Zambia nchini Judith Kangoma (kulia) jana mjini Dar es salaam wakati wa kongamano la siku moja la wanataalum liloandaliwa maalum na Chuo Kikuu cha Dar es salaam la kutambua mchango wake kitaalum wa Profesa alioutoa ndani na nje Tanzania.
Mwapachu- Katibu Mkuu zamani wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Balozi Juma Mwapachu akichangia mada jana mjini Dar es saam wakati wa kongamano la siku moja la wanataalum liloandaliwa maalum na Chuo Kikuu cha Dar es salaam la kutambua mchango wa Profesa Goran Hyden alioutoa ndani na nje Tanzania.Kulia ni Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Profesa Rwekaza Mukanda.