Mei Day Zanzibar katika matukio ya Picha
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiwapungia mkono wafanyakazi wakati
akipokea maandamano ya wafanyakazi wa Taasisi mbali mbali za Serikali
na Binafsi,katika maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani (Meyday)
yaliyofanyika katika viwanja vya Ukumbi wa Bwawani Hotel Mjini
Zanzibar jana.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Wafanyakazi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali,
wakipita mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) akiwa mgeni rasmi
katika Sherehe za kilele cha Maadhimisho ya siku ya wafanyakazi
Duniani huko viwanja vya Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja
zilizofanyika jana.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]