VIONGOZI WA DINI WAPIGWA MSASA KUHUSU SENSA YA WATU NA MAKAZI 2012

Katibu Mkuu wa Wizara

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Ramadhani Khijjah akizungumza na viongozi mbalimbali wa dini kuelezea umuhimu na ushiriki wao katika kufanikisha sensa ya watu na makazi itakayofanyika kitaifa mwezi Agosti mwaka huu wakati wa mkutano wa viongozi wa dini unaoendelea jijini Dar es salaam

Viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini nchini wakifuatilia kwa makini hotuba ya Katibu mkuu wa Wizara ya Fedha na uchumi Ramadhani Khijjah alipokuwa akizungumzia umuhimu wa sensa ya watu na makazi 2012 na namna serikali ilivyojipanga kukamilisha zoezi hilo kwa ufanisi.

wakifuatilia

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Ramadhani Khijjah (kushoto) akiandika maswali yaliyoulizwa na viongozi wa dini kuhusu namna serikali ilivyojipanga kukamilisha sensa ya watu na makazi itakayofanyika mwezi Agosti 2012. Wengine ni mkurugenzi mkuu wa ofisi ya taifa ya takwimu Dkt. Albina Chuwa (katikati) na kamishna wa sensa Bi. Hajjat Amina Mrisho.

wakizungumza jambo